GUARDIOLA APATA USHINDI WA KWANZA MBELE YA BORRUSSIA DORTMUND
Mkufunzi mpya wa Manchester City,Pep
Guardiola, amesajili ushindi wake wa kwanza tangu atue Manchester City
baada ya kuwaongoza mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu ya Uingereza
kuwalaza Borussia Dortmund katika kinyang'anyiro cha kutafuta mabingwa
wa vilabu vya kimataifa huko China.
Kipa chipukizi wa Man City
Angus Gunn, 20, aliokoa mkwaju wa penalti wa Mikel Morino na
kuwahakikishia vijana wa Pep ushindi wa mabao 6-5.Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Longgang ulioko Shenzhen ilikuwa imeishia sare ya 1-1 katika muda wa kawaida.
Sergio Aguero alikuwa ameiweka Man City kifua mbele mapema katika mechi hiyo lakini mshambulizi chipukizi wa Dortmund Christian Pulisic, mwenye umri wa miaka 17, kuwasawazishia wajerumani hao katika muda wa majeruhi.
Hii ndio ilikuwa mechi ya kwanza kwa Man City baada ya mechi iliyokuwa imepangwa awali dhidi ya vibonde wao wa jadi kutoka Uingereza Manchester United kuahirishwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mjini Beijing.
Post a Comment