KOFFI OLOMIDE AENDELEA KUSOTA JELA BAADA YA WANASHERIA WAKE KUKOSA DHAMANA
Mwanamuziki Koffi Olomide ameendelea kuwekwa kizuizini huku wanasheria wake wakishindwa kupata dhamana kwa nyota huyo anaetamba na kibao chake cha Ekotite,ambae ameshatakiwa kwa kumpiga mmoja ya wachezaji wake nchini Kenya.
Tukio hili lilirekodiwa na limesambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. Msanii huyu maarufu wa Congo atasalia jela kwa siku zaidi ya kumi na tano. Uamuzi ambo umepingwa na mwanasheria wake Ruffin Lukoo.
Koffi Olomide, alikamatwa jijini Kinshasa kwa kosa la kumpiga teke mnenguaji wake wa kike jijini Nairobi nchini Kenya mwishoni mwa juma lililopita.
Masaibu ya Olomide yameendelea kushuhudiwa kwa juma la pili baada ya kukamatwa na kufukuzwa nchini Kenya kutokana na tukio hilo, na tamasha lake kusitishwa.
Polisi nchini DRC wanasema mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 60 anashikiliwa kwa mahojiano zaidi kutokana na tukio la Nairobi.
Jumapili iliyopita, Olomide alihojiwa na Televisheni moja nchini humo akiomba msamaha kwa kitendo alichofanya.
Post a Comment