MWALUSAKO ASEMA UKOSEFU WA UMAKINI WA WASHAMBULIAJI NA MABEKI WA YANGA NDIO UMEWAGHARIM KUTOFANYA VIZURI KWA TIMU HIYO KWENYE MECHI ZA KIMATAIFA


Baada ya kushindwa kutamba katika michuano ya kimataifa barani Afrika leo hii aliyekua katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Laulence Mwalusako amesema kwamba tatizo kubwa ambalo limewagharimu Yanga katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ni kukosa uzoefu wa michuano ya hiyo pamoja na safu ya ushambuliaji kutokua makini

Mwalusako amesema kwamba Yanga inastahili kupongezwa kwa hatua ambayo imefika lkn kocha mkuu anatakiwa kuboresha kikosi chake kwenye nafasi ya beki na ushambuliaji ambazo sehemu hizo zimeonekana kupwaya hata sehemu ya kiungo

Amesema kwamba katika mechi ya jana dhidi ya Medeama ya nchini Ghana ambapo wawakilishi hao wa Tanzania walipoteza kwa kufungwa kwa jumla ya mabao 3-1 kumekua hakuna uelewano mzuri kwenye nafasi ya ulinzi na kusababisha kufungwa magoli ya kizembe huku akimpa sifa Andrew Dante aliyeingia kipindi cha pili kuchukua mikoba ya Cavin Yondan kua alicheza vizuri

Hata hivyo Mwalusako amesema kwamba vilabu vya Tanzania hasa vinavyoshiriki michuano ya kimataifa vinatakiwa kusajili wachezaji ambao wana sifa ya kumudu michuano hiyo kwani wengi wao ambao wamesajiliwa wameshindwa kuonyesha uwezo wa kuvisaidia vilabu vyao kwenye michuano hiyo.

No comments