KISA CHIRWA AKILIMALI AMVAA HANS DER PLUIJM


Katibu wa baraza la wazee wa Yanga Ibrahim Akilimali amesema kwamba kocha mkuu wa klabu hiyo Hans Van Pluijm alifanya makosa kumuanzisha mchezaji Obrey Chirwa katika mechi dhidi ya TP Mazembe na Medeama kwa kua mchezaji huyo alikua hajafahamu mfumo wa kikosi cha timu hiyo

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT, Akilimali mesema kwamba Chirwa ni moja ya wachezaji wazuri lkn hakustahili kucheza katika mechi ile ya kwanza kwa upande wake kutokana na ugeni wake hivyo imempa wakati mgumu kwa yeye kufanikiwa kucheza kwa kiwango chake


Aidha amedai kua hata kauli yake ambayo aliitoa baada ya mechi dhidi ya TP Mazembe katika mechi ambayo imechezwa kwenye uwanja wa Taifa kwa kusema kwamba Chirwa si mchezaji wa kiwango cha kuchezea Yanga ni fumbo ambalo amelitumia kuzungumza kwa uma lkn dhumuni lake ni ujumbe ufike kwa kocha mkuu


Amedai kua kwa malezi ambayo wamekulia si vyema kumesema baba mbele ya watoto hivyo aliamua kumsema Chirwa kwa kua yeye yupo chini ya kocha mkuu na isengekua vyema kumesema Hans hadharani


Hata hivyo amesema kwamba yeye bado anaridhishwa na kiwango cha Chirwa ambae amesajiliwa kutoka nchin Zimbabwe kwani ana matumaini makubwa ya mchezaji huyo kuwasaidia kwenye michuano mbalimbali

No comments