AKILIMALI AHUSISHA NA IMANI ZA KISHIRIKINA KWA YANGA KUTOFANYA VIZURI HAPA NYUMBANI KWA MECHI ZA KIMATAIFA


Katibu wa baraza la wazee wa Yanga,Ibrahim Akilimali amesema kwamba bado wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa hasa kuelekea kwenye mechi yao ya kesho dhidi ya Medeama ya nchini Ghana

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,Akilimali amesema kwamba timu yao hua ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri ugenini kuliko hapa nyumbani baada ya kusema kwamba wakicheza hapa nyumbani wanakumbana na ushirikina kutoka kwa watu ambao hawapendi kuona timu hiyo ina fanikiwa zaidi

Amesema kwamba kutokana na ubora wa kikosi chao anaamini watapata ushindi mbele ya Medeama ambapo katika mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa timu hizo zilifungana bao 1-1.

No comments