AIRTEL YAKABIDHI VIFAA KWA TIMU ZA VIJANA KWA AJILI YA MASHINDANO YA AIRTEL RISING STAR
Kampuni ya simu za mkononi Airtel,leo hii imekabidhi vifaa
vya michezo zikiwemo jezi kwa timu ambazo zinashiriki michuano ya vijana ya
Airtel Rising Star inayotaraji kuanza kutimua vumbi siku ya jumamosi kwa ngazi
ya mkoa
Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,meneja uhusiano wa Airtel
Jackson Mbano amesema kwamba vifaa hivyo vya michezo ambavyo vitatumika katika
mashindano hayo kwa timu zote vina thamani ya shilingi milioni 200
Mbando amesema kwamba mgeni rasmi katika ufunguzi wa
mashindano hayo ambayo yatazinduliwa kwenye uwanja wa Karume katika makao makuu
ya TFF anatarajiwa kua mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda sambamba na
viongozi wengine wa mpira wa miguu hapa nchini.
Amesema kwamba dhamira yao ni kuona kampuni ya Airtel
inasaidia kukuza vipaji vya vijana kupitia sekta ya michezo kama ambavyo
wamekua wakifanya kipindi chote ambacho wamekua wakidhamini mashindano ambayo
yamefanikiwa kuibua vipaji bora vya vijana ambao kwa sasa wamekua msada mkubwa
kwa timu za taifa hasa katika kikosi cha Serengeti boys.
Kwa upande wake katibu mkuu wa TFF,Mwesigwa Selestine
ameishukuru kampuni hiyo kwa kuendelea kutoa udhamini kwa timu za vijana ambapo
kwa mujibu wa taarifa yake amesema kwamba Airtel imekua msada mkubwa kwa kuibua
vipaji vya vijana katika sekta ya michezo hivyo amewataka wadau wengine nao
waige mfano huo ili kuendelea kuleta chachu ya maendeleo ya soka hapa nchini
Mwesigwa amesema kwamba jambo ambalo linafanywa na Airtel ni
jambo zuri linalotakiwa kuigwa na makampuni mengine kwa ajili ya kuwekeza katika
mashindano mbalimbali,pia amewataka mashabiki wa mpira kuendelea kutumia mtandao
wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kununua vocha kwani kufanya hivyo ni sawa na
kuipa sapoti kampuni hiyo iendelee kudhamini mashindano hayo ya Airtel Rising
Star.
Post a Comment