YANGA YAENDELEA KUBORONGA KWENYE MECHI ZA SHIRIKISHO


Matumaini ya timu ya Yanga kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika yameendelea kua finyu baada ya usiku huu kukubali kupokea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Medeama katika mechi ambayo imechezwa nchini Ghana

Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kushika mkia katika msimamo wa kundi A linaloongozwa na TP Mazembe wenye alama saba wakifuatiwa na Mo Bejaia na Medeama ambazo kila mmoja amefikisha alama tano.

Katika mechi ya leo bao la kufutia machozi kwa upande wa Yanga limefungwa na Saimon Msuva kwa mkwaju wa penati iliyosababishwa na Obrey Chirwa aliyechezewa mazambi ndani ya box

Mabao ya Medeama yamefungwa na Daniel Amoah na Abbas Mohamed ambae ametupia kambani mabao 2 mguu mwake.

No comments