MALINZI AZINDUA RASMI MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amefungua rasmi mashindano ya kuibua na kukuza vipaji vya mpira wa miguu Airtel Rising Star ufunguzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya Barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT katika ufunguzi huo,Malinzi ameipongeza kampuni ya Airtel kwa kujikita zaidi kwenye soka la vijana kwa msimu wa sita ambapo kupitia mashindano hayo yamefanikiwa kuibua vipaji vya vijana.


Aidha Malinzi amewataka viongozi wa vyama vya mpira kua makini na umri wa wachezaji katika mashindano husika kwani udanganyifu wowote ambao utajitokeza kwenye mashindano ya kimataifa utaleta hasara kwa nchi.


Kwa upande wake meneja wa Airtel kanda ya Dar es salaam,Fredrick Mwakitangwe amesema kwamba lengo la kampuni hiyo ni kuibua vipaji vya vijana hivyo ni vyema wadau wa soka wakazingatia umri wa wachezaji katika mashindano hayo ili kuleta tija ya maendeleo ya mpira wa miguu.

Amesema kwamba dhamira yao kuu ni kuona Tanzania inapiga hatua kwenye maendeleo ya soka na ndio maana kampuni ya Airtel imeamua kujikita zaidi kwa vijana ambapo makampuni mengi hua yanashindwa kuwekeza sehemu hiyo.

Katika hatua nyingine aliyewai kua katibu mkuu wa kamati ya uchaguzi ndani ya klabu ya Yanga,Francis Kaswahili amesema kwamba jambo ambalo linafanywa na kampuni ya Airtel ni jambo la kuigwa kwani siku zote msingi wa soka unaanzia ngazi ya vijana.

Kaswahili amesema kwamba hata awali klabu ya Yanga ilikua na mfumo bora wa kukuza vijana na ikapelekea kua na timu bora ambayo ilileta ushindani wa hali ya juu kwenye mashindano mbalimbali.

No comments