MOHAMED DEWJI AKILI KUTAKA KUWEKAZA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 20 KATIKA KLABU YA SIMBA


Bilionea kijana, Mohammed Dewji amesema kwamba yupo tayari kuwekeza kiasi cha shilingi bilioni 20 katika klabu ya Simba ili kununua hisa za asilimia 51 kwenye klabu hiyo

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii Dewji amesema kwamba ameamua kufanya hivyo baada ya kuona timu hiyo kwa sasa haina mwelekeo wa kiushindani na timu nyingine za hapa nyumbani za Yanga na Azam hasa katika swala zima la bajeti za uendeshaji

Amesema kwamba Simba kwa sasa inashindwa kushindwana na klabu ya Azam ambayo imeanzishwa hivi karibuni huku ikizidiwa kete na mahasimu wao wa jadi hasa linapofika swala la usajili wa wachezaji na ushiriki wa timu hiyo kwenye michuano mbalimbali ya kiamataifa

Katika hatua nyingine Dewji ametoa mchanganuo wa fedha hizo za shilingi bilioni 20 ambapo amesema kwamba fedha hizo zitapelekwa benki kwa ajili ya kuikopesha serikali ili na wao kufaidika kwa asilimia itakayopatikana

Amesema kwamba faida itakayopatikana itatumika kwa lengo la kufanya usajili wa wachezaji wazuri,kujenga uwanja na kuwalipa vizuri wachezaji mishahara yao ili waanze kupamba na wapinzani wao ambao wanaonekana kupiga hatua katika soka la ushindani

No comments