SIMBA WASITISHA MPANGO WA KWENDA FIFA


Kuna taarifa kwa sasa inazagaa kwenye mitandao ya kijamii ikisema kwamba uongozi wa timu ya soka ya Simba kupitia kwa raisi wa klabu hiyo Evans Aveva umesema kwamba umesitisha mpango wake mara moja wa kupeleka barua ya kukata rufaa FIFA dhidi ya maamuzi yaliyotolewa na TFF kuhusu pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar.

Katika taarifa iliyotolewa na Aveva inasema kwamba uongozi umekubaliana kupokea zawadi ya mshindi wa pili waliyoipata baada ya  kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Aidha klabu hiyo imeipongeza timu ya Yanga kwa kufanikiwa kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara huku wakiomba radhi kwa lolote ambalo walilifanya kwa namna nyingine.

Bado MWANDIKE.BLOGSPOT inaendelea kupata ukweli wa ndani juu ya taarifa hiyo.

No comments