KEN ALLY AJIUNGA NA SINGIDA UNITED

Kiungo mahiri wa timu ya soka ya Mbeya City Ken Ally amejiunga rasmi na klabu ya Singida United kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Ken Ally ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wakiwindwa vikali na vilabu vikubwa vya hapa nchini Simba na Yanga hivyo kusaini Singida United ni pigo kwao kwani wamekatisha mipango yao.

Singida United ni miongoni mwa timu ambazo zimeanza kutazamwa na wadau wa soka kwamamba huenda wakaleta mapinduzi katika soka hapa nchini hii inatokana na mipango yao ikiwemo usajili wa wachezaji wa kigeni.

No comments