MSAFARA WA RUVU SHOOTING WAPATA AJALI


Msafara wa timu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani umepata ajali mbele kidogo ya mji wa Singida wakiwa safarini kurejea jijini Dar es salaam baada ya kukamilisha mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Stend United.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa walioshuhudia ajali hiyo walisema kwamba chanjo cha ajali hiyo ni baada ya kupasuka kwa taili wakati gali hilo likiwa kwenye mwendo kasi na kusababisha gari kuhama njia na kuparamia miti iliyokuwa jirani.

Hata hivyo imeelezwa kuwa  hakuna mtu yeyote aliyeumia zaidi ingawa kuna mchezaji mmoja amepatwa na majeraha ya kawaida.

No comments