MFUNGAJI BORA WA LIGI KUU APINGANA NA TFF

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Ruvu Shooting Abdulrahman Mussa ambae ni miongoni mwa vinara wa ufungaji wa magoli katika msimu wa ligi kuu ya Tanzania bara uliomalizika wiki iliyopita amesema kwamba yeye ndie alistahili kuwa mfungaji bora pekee wa ligi licha ya kulingana na Simon Msuva.

Abdulrahman alisema kwamba anajiuliza je TFF imetumia vigezo gani hadi kufikia maamuzi ya kupewa zawadi sawa na Simon Msuva ambae pia nae amefikisha jumla ya magoli 14.

Alisema kwamba kwa upande wake anaamini yeye ndie alifaa kuchukua zawadi hiyo pekee kwani alifunga magoli mengi ya kujitengenezea tofauti na mwenzake aliyefunga magoli mengi kwa kutengenezewa na wachezaji wenzake.

Aidha alisema kwamba pia Msuva alishinda magoli mengi ya penati tofauti na ilivyo kwake hivyo anaamini hicho kilikuwa kigezo tosha cha kunyakuwa tuzo hiyo.

Hata hivyo amedai kuwa kwa kuwa TFF imeamua hivyo basi kwake hatakuwa na kinyongo chochote kwani anaamini mpira ndio kazi yake na atahakikisha atafanya vizuri zaidi kwenye msimu ujao wa ligi.

No comments