YANGA YAWASILI MKOANI ARUSHA

Kikosi cha timu ya Yanga tayari kimeshawasili mkoani Arusha ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya klabu hiyo kwa lengo la kwenda kulitembeza kombe kwa mashabiki wao.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Chars Boniphace Mkwasa alisema kwamba kikosi hicho kinataraji kucheza mchezo wa kirafiki hapo kesho na timu ya AFC ya Arusha kabla ya kucheza na timu nyingine ya mkoa huo.

Aidha Mkwasa alisema kwamba kwa sasa uongozi upo katika mikakati kabambe ya kuhakiksha wanafanya usajili mzuri ili kupata kikosi bora cha msimu ujao.

Alisema kwamba pia wanataraji kuwatumia wachezaji ambao hawakupata nafasi katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara kwenye michuano ya SportPesa inayotaraji kuanza mwezi ujao.

No comments