URUGUAY YAICHAPA JAPANI KOMBE LA DUNIA

Michuano ya kombe la dunia la vijana chini ya umri wa miaka 20 inaendelea kushika kasi huko nchini Korea ya kusini ikiwa katika ngazi ya makundi.
Katika michezo ya kundi C wawakilishi wa Afrika timu ya Zambia walipata ushindi mabao 4-2 dhidi ya timu ya Iran. Nao Costa Rica wakatoshana nguvu na Ureno kwa Sare ya bao 1-1.
Kwenye kundi D Afrika ya kusini walichapwa na Italia kwa mabao 2-0, huku Uruguay wakiwafunga Japani kwa 2-0.
Michuano hiyo inaendelea tena leo katika kundi E Ufaransa watacheza na Vietnam, na New Zealand wakipepetana na Honduras.
Katika kundi F Ecuador wataonyesha ubavu na Saudi Arabia, huku Senegal wakicheza na Marekani.

No comments