SHAZZY SHERY ATAMBA KUITENDEA HAKI BONGO FREVA

Msanii wa bongo freva Shazzy Shery ametamba kufanya vizuri kwenye soko la muziki wa bongo baada ya kuanza kupokelewa vizuri kazi zake na wadau wa muziki huo hapa nchini.

Shazzy alisema kwamba anaamini ubora wa nyimbo zake ndio utamfanya yeye ajulikane zaidi kwenye tasnia ya muziki.

Alisema kwamba kwa sasa tayari amesharekodi nyimbo tatu ambazo zinaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio huku wadau wakizipa sapoti kubwa.

Msanii huyo ambae aliwai kufanya kazi na bendi mbalimbali za muziki wa dansi hapa nchini leo hii anataraji kuitambulisha ngoma yake mpya iitwayo Sina Noma katika kituo cha radio cha Choice FM kuanzia mishale ya saa moja hadi saa tatu usiku akiwa chini ya DJ Muba.

No comments