TFF YAKATAA KUZUNGUMZIA SWALA LA SIMBA FIFA

Wakati uongozi wa klabu ya Simba ukiendelea kusisitiza kuwa bado wanasubiri taarifa kutoka FIFA baada ya kuwasilisha malalamiko yao ya kupokwa pointi tatu,leo hii shirikisho la mpira wa miguu TFF limesema kwamba kwa wakati huu hawawezi kuzungumzia maswala ya Simba kwenda FIFA.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema kwamba maswala hayo yatabaki kwa klabu ya Simba na wao hawatakuwa na sababu za kuzungumza juu ya jambo hilo kwani halipo mikononi mwao.

No comments