MWAKYEMBE AONGOZA MAPOKEZI YA SERENGETI BOYS
Kikosi cha timu ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys kimewasili salama leo hii jijini Dar es salaam kutoka nchini Gabon kilipokuwa kinashiriki fainali za vijana walio na umri chini ya miaka 17.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe aliwaongoza watanzania katika mapokezi hayo ya vijana waliondoshwa kwenye michuano hiyo na timu ya Niger baada ya kukubali kufungwa kwa jumla ya bao 1-0.
Mwakyembe amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kushiriki kwao michuano hiyo kwa mara ya kwanza na kuwaambia kuwa kuondoshwa kwao ni mwanzo mpya ya kufanya maandalizi kwa ajili ya kuitumikia Ngorongoro Herous.
Post a Comment