MASHABIKI ELFU 23 KULISHUHUDIA PAMBANO LA SIMBA NA MBAO FC

Uongozi wa chama cha soka mkoa wa Dodoma DOREFA,umesema kwamba kwa ujumla maandalizi kuelekea kwenye fainali ya michuano ya FA ambayo itawakutanisha Simba na Mbao FC kwa asilimia kubwa yameshakamilika.

Mwenyekiti wa chama hicho Mlamu Ng'ambi alisema kwamba tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya kesho katika vituo mbalimbali ambavyo wamevitangaza na kiingilio cha chini ni shilingi elfu tano.

Ng'ambi alisema kwamba kwa sasa wa uwanja tayari umeshakarabatiwa vizuri ikiwemo kupunguza nyasi za uwanjani pamoja na marekebisho mengine ambayo yalipaswa kufanyiwa ukarabati.

Aidha alisema kwamba kwa upande wao wamepanga utaratibu wa kutengeza tiketi elfu ishirini na tatu ambazo ndio idadi ya mashabiki watakaopata fursa ya kulishuhudia pambano hilo na hakutakuwa na ongezeko la tiketi.

No comments