MWAMBUSI;TOTO AFRICANS WALIKUWA WAZURI ZAIDI LEO HII

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Yanga,Juma Mwambusi amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Toto Africans ya jijini Mwanza.

Mwambusi alisema kwamba mechi ya leo imekuwa na ushindani zaidi kwa upande wao kwani dhamira yao ilikuwa ni kuibuka ushindi ili watimize azma yao ya kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa mara ya tatu mfululizo.

Alisema kwamba mechi ya leo ilikuwa na ushindani wa hali ya juu hasa baada ya wapinzani wao kujilinda zaidi ambapo hali hiyo iliwapa wakati mgumu wachezaji wake katika upachikaji wa mabao.

Aidha alisema kwamba baada ya kubaini mbinu hizo kwa upande wa wapinzani ndipo wakaamua kufanya mabadiliko kadhaa ambayo yaliwapa chachu ya kupata goli lililofungwa na mchezaji Amisi Tambwe.

No comments