YANGA YAIZIDI SIMBA UDHAMINI WA SPORTPESA
Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa imeingia mkataba wa kuidhamini klabu ya Yanga kwa muda wa miaka mitano,mkataba wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tano.
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii mkurugenzi wa utawala wa SportPesa,Tarimba Abasi amesema kwamba wameingia mkataba na klabu hiyo wakiwa na nia njema ya kuleta maendeleo katika mpira wa miguu.
Alisema kwamba anaamini mkataba huo wa miaka mitano utaleta chachu kwa klabu hasa kuweza kujiendesha kwa utulivu mkubwa kwenye michuano mbalimbali.
Aidha alisema kwamba kwa mwaka wa kwanza Yanga itapata fedha kiasi cha shilingi milioni 950 ambayo italipwa kwa kila baada ya miezi mitatu huku pia mkataba huo ukiwa na ongezeko la asilimia tano kwa kila mwaka.
Hata hivyo ameongeza kuwa kuhusu swala la motisha kwa klabu endapo timu itakuwa bingwa wa ligi na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa jambo hilo litaenda sawa kama ilivyo kwa klabu ya Simba.
Simba kwa upande wao walikuwa wa kwanza kuingia udhamini wa miaka mitano ambao una thamani ya bilioni 4.9 na kampuni hiyo yenye chachu ya kuleta maendeleo ya mpira wa miguu.
Post a Comment