WANACHAMA SIMBA WAMPONGEZA HANS POPE

Baada ya mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Simba,Zacharia Hans Pope kuamua kurejea kundini kuendelea na majukumu ndani ya klabu hiyo,leo hii baadhi ya wanachama wa Simba wamempongeza kwa hatua aliyoifanya ya kuungana na wenzake kwa mara nyingine.

Mmoja wa wanachama wa timu hiyo aliyejulikana kwa jina la Haruna Nazi amesema kwamba kitendo alichokifanya Hans Pope cha kuamua kubadili mawazo yake ya kujiuzulu ni cha kiungwana kwani yeye ni miongoni mwa viongozi wanaohitajika ndani ya Simba.

Aidha Nazi amewaasa viongozi wa klabu hiyo kuwa makini kwa kipindi hiki kwa kuachana na migogoro ambayo haina msingi kwani dhamira yao ni kuona wanafanikiwa kuwa mabingwa wa kombe la FA ili nao wapate nafasi ya uwakilishi wa nchi kwenye michuano ya kimataifa.

No comments