MTAZAMO WA MASHABIKI KUHUSU BINGWA WA LIGI KUU

Wakati uongozi wa timu ya soka ya Simba ukiamini kuwa bado wana nafasi ya kuwa mabingwa wa ligi ya Tanzania bara kwa msimu huu,asilimia kubwa ya mashabiki wa mpira wa miguu wanasema kwamba jambo hilo ni gumu kutokea kwa timu hiyo kuchukua ubingwa.

Wadau hao walisema kwamba ni vigumu kwa timu ya Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi wa zaidi ya magoli 10 mbele ya timu ya Mwadui katika mchezo unaoataraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku wakiombea Yanga ifungwe kwenye mechi yao dhidi ya Mbao FC.

Simba kwa sasa ina jumla ya alama 65 ikiwa kwenye nafasi ya pili huku Yanga ikiwa na alama 68 wakishika nafasi ya kwanza na kila timu imesaliwa na mchezo mmoja ambao michezo hiyo itapigwa leo hii.

Yanga kwa upande wake anahitaji pointi moja kujihakikishia ubingwa wa ligi hiyo kwani itawafanya kutimiza alama 69 zitakazowafanya Simba washindwe kuzifikia.

Ligi hiyo ya Tanzania bara inataraji kufikia tamati leo hii kwa timu zote kucheza mechi zao za mwisho katika viwanja tofauti.

Mechi hizo ni pamoja na Simba itamenyana na Mwadui FC kwenye uwanja wa Taifa,Azam FC itaikaribisha Kagera Sugar katika uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi.

Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya Tanzania Prison itakuwa nyumbani kupambana na Afrika Lyon wakati kwenye uwanja wa Manungu Turiania Mtibwa Sugar itakwaana na Toto Africans.

Mechi nyingine Majimaji itacheza na Mbeya City mkoani Ruvuma,Stend United itamenyana na Ruvu Shooting,Ndanda na Jkt Ruvu zitakwaana mkoani Mtwara.

Mchezo mwingine ambao unataraji kuwa na mashabiki wengi ni utakaowakutanisha Mbao FC na Yanga mechi itakayopigwa mkoani Mwanza.

Hata hivyo mbali na wadau hao kuzungumzia swala la ubingwa lakini pia bado wanashauku ya kuzijua timu mbili ambazo zitaungana na Jkt Ruvu zitakazoshuka daraja msimu huu.

No comments