KAGERA SUGAR WAIPONGEZA KAMATI YA TFF
Uongozi wa timu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera umeridhishwa na maamuzi ya kamati ya TFF baada ya kamati hiyo kuchukua jukumu la kuifuta kadi nyekundu aliyepewa mchezaji wao Mbaraka Yusuph wakati wa pambano lao dhidi ya Yanga.
Mwenyekiti wa Kagera Sugar,Hamis Madaki alisema kwamba kwa upande wao kama uongozi umezipokea taarifa hizo kwa uzuri kabisa kwani walibaini kuwa kadi aliyopewa mchezaji wao haikuwa halali na ndio maana wakaamua kuwasilisha malalamiko yao.
Alisema kwamba hata hatua iliyochukuliwa ya kumuondosha mwamuzi Ngole Mwangole kwenye orodha ya waamuzi wa ligi kuu ni sahihi kwani ameshindwa kufuata sheria 17 za soka.
Post a Comment