TP MAZEMBE YAANZA KWA USHINDI MICHUANO YA CAF

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambayo ndio mabingwa watetezi wa taji la klabu bingwa barani Afrika ilianza kwa sare ya kutofungana katika mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Saint George ya Ethiopia mwishoni mwa juma lililopita.

Hata hivyo, Esperance de Tunis ya Tunisia ikicheza nyumbani mjini Rades, ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya AS Vita Club ya DRC.
Kundi hili linaongozwa na Esperance de Tunis kwa alama 3, ikifuatwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa alama moja.
Mechi ya mzunguko wa pili zitapigwa tarehe 23 mwezi huu wa Mei.
Saint George itakuwa nyumbani kumenyana na Esperance de Tunis, huku AS Vita Club ikipambana na Mamelodi Sundowns.
Matokeo mengine:
Kundi A
Etoile du Sahel 5-0 Ferroviario Beira
Al Hilal 1-1 Al-Merrikh
Kundi B
USM Alger 3-0 Al-Ahli Tripoli
Zamalek 2-CAPS United
Kundi D
Wydad Casablanca 2-0 Coton Sport
Al-Ahly 0-0 Zanaco
Katika michuano ya Shirikisho, klabu ya KCCA ya Uganda ilianza vibaya ugenini baada ya kufungwa na FUS Rabat ya Morocco mabao 3-0.
Club Africain ya Tunisia nayo ilianza vema kwa kushinda Rivers United ya Nigeria mabao 3-1.
Mabingwa watetezi TP Mazembe ya DRC ambao wapo katika kundi D, walianza vema baada ya kuishinda CF Mounana ya Gabon kwa mabao 2-0, huku SuperSport United ya Afrika Kusini ikitoka sare ya mabao 2-2 na Horoya ya Guinea.
Matokeo mengine:
Kundi la C
ZESCO United 1-0 Smouha
Recreativo do Libolo 1-0 Al Hilal Al-Ubayyid
Kundi B:
CS Sfaxien 1-0 Mbabane Swallows
Platinum Stars 1-1 MC Alger

No comments