LWANDAMINA AMUANZISHA SIMON MSUVA MECHI YA MBAO

Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina leo hii amemuanzisha winga machachali wa timu hiyo Simon Msuva katika kikosi cha kwanza kitakachopambana na Mbao FC leo hii katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotaraji kupigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Msuva hakutarajiwa kucheza mechi ya hii leo hasa baada ya kupata majeruhi katika mechi dhidi ya Mbeya City na pia kukosa mchezo dhidi ya Toto Africans.

Blia shaka Msuva ana chachu ya kufunga goli leo hii ili afanikiwe kutwaa tuzo ya mfungaji bora kwani hadi sasa yeye ndio anaongoza kwa ufungaji akiwa na jumla ya magoli 14.

KIKOSI KAMILI CHA YANGA SC LEO DHIDI YA MBAO FC
1. Beno Kakolanya
2. Juma Abdul
3. Oscar Joshua
4. Nadir Haroub
5. Vincent Bossou
6. Thabani Kamusoko
7.Saimon Msuva
8. Justine Zulu
9. Obrey Chirwa
10. Haruna Niyonzima
11. Geofrey Mwashuiya
Akiba
Deogratius Munishi, Hassani Kessy, Pato Ngonyani, Mateo Antony , Deusi Kaseke na Emanuel Martin.

No comments