TASMA WAJIPONGEZA WENYEWE

Kuelekea kumalizika kwa ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu,chama caha madaktari wa tiba za wanamichezo Tanzania TASMA kimethibitisha kufanikiwa kumaliza vyema katika utoaji wa tiba kwa wachezaji  kutokana na kutokuwepo kwa matatizo makubwa kwa wacheza katika msimu huu.

Katibu wa chama hicho Nasoro Ally Matuzya alisema kwamba kwanza wanashukuru hadi kufikia sasa hakuna mchezaji ambaye amepatwa na jeraha kubwa hivyo kwao ni jambo la faraja.

Aidha alisema kwamba chama chao mwezi ujao mwaka huu kinaelekea katika uchaguzi mkuu ambao utawawezesha kupata viongozi wapya wa  chama hicho ambapo taratibu zote ziko mwishoni kumalizika.

Matuzya alisema kwamba wanaamini kutokana na changamoto nyingi ambazo zimejitokeza katika ligi kuu soka Tanzania Bara kwa msimu huu basi viongozi waonaokuja wataweza kumalizia yale ambayo yaliwekwa kwa ajili ya kumaliza na kuondoa changamoto hizo.

No comments