WILLIAM LUCIAN GALLAS NA MOHAMED MKOPI WAFUNGIWA MWAKA MMOJA KUTOCHEZA SOKA


Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF kupitia Kamati yake ya sheria na hadhi za wachezaji imetoa tahadahri kwa vilabu vya Majimaji ya Songea,Mwadui ya Shinyanga,Mbeya City,Afrika Lyoni pamoja na Mbao FC kutowatumia wachezaji ambao wameoneka kua na matatizo kwenye mikataba yao baadhi yao wakijisajili kwenye vilabu viwili tofauti kwa msimu mmoja.

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba kwa upande wa timu ya majimaji shirikisho linatoa tahadhali klabu hiyo kutomtumia mchezaji Georg Mpole kwa sababu amefungiwa mwaka mmoja baada ya kujisajili katika vilabu viwili vya ligi kuu ya Tanzania bara.

Aidha beki wa zamani wa timu ya Simba,William Lucian "Gallas"  na kiungo wa Tanzania Prisons Mohamed Mkopi nao wamefungiwa mwaka mmoja  kutocheza soka kwa kosa la kufanya udanganyifu wa kujisajili kwenye vilabu viwili

Lucas amesema kwamba Gallas amefanya udanganyifu wa kujisajili Ndanda na Mwadui huku Mkopi akisajiliwa na Mbeya city sambamba na Tanzania Prisons.

No comments