KIFUKWE ASEMA HAWAJAPOKEA TAARIFA RASMI ZA KUJIUZULU YANGA KWA MANJI


Mjumbe wa baraza la wadhamini wa klabu ya Yanga Fransis Kifukwe amesema kwamba bado hawajapata taarifa rasmi juu ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuphu Manji na kusitisha mpango wake wa kutaka kuikodisha timu kwa miaka 10.

Kifukwe amesema kwamba hizo taarifa yeye anazisikia kwa baadhi ya watu lkn kwa upande wake kama mjumbe wa baraza la wadhamini taarifa hizo hazipo.

Amesema kwamba kwa upande wao watakua tayari kulizungumzia jambo hilo pindi watakapopata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kla hiyo ya YANGA.

No comments