TOTO AFRICA YAJINASIBU KUFANYA VIZURI MSIMU UJAO


Uongozi wa timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kinaendela vizuri na maandali ya kujiwinda na msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara

Msemaji wa timu hiyo Cuthbert Japhet ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba hapo kesho kikosi hicho kinataraji kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya Black Ego ya nchini Burundi mchezo ambao utachezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba

Amesema kwamba wanaamini msimu ujao kikosi chao kitafanya vizuri hasa kutokana na maandalizi ambayo wanayapata chini ya kocha mkuu Logasian Kaijage.

No comments