YANGA YAIPIGA KO SIMBA KUHUSU SAKATA LA HASANI KESSY


Kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji ya shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF imemuidhinisha mchezaji Hassan Ramadhani Kessy kuichezea klabu ya Yanga baada ya kamati hiyo kuamua kutoa maamuzi hayo ambayo waliketi kwa ajili ya kujadili maswala mbalimbali ya wachezaji wenye matatizo ya usajili hapo jana.

Akiongeana na MWANDIKE.BLOGSPORT,Ofsa habari wa TFF Alfred Lucas amesema kwamba kama imemuidhinisha Kessy kuichezea Yanga ili kulinda kiwango cha mchezaji na jambo lingine kwamba mchezaji huyo usajili wake upo upande mmoja.

Amesema kwamba kuhusiana na swala la klabu ya Simba juu ya madai yao ya fedha baada ya mchezaji huyo kuvunja mkataba shirikisho hilo limesema kwamba Simba italipwa fedha zake lkn kamati husika ya TFF itakaa na kujadili kuhusiana na kiwango ambacho Simba wanakihitaji kama kina lingana na sheria za mkataba.

"Simba wao wanataka kulipwa dola 60 ambazo zaidi ya shilingi milioni 120 za Tanzania sasa je hizo pesa wanazotaka Simba zinaendana na muda wa mkataba wa mchezi ambao ulisalia,lkn Simba watalipwa fedha zao baada ya pande hizo kukaa na kujadiliana"alisema Lucasi.

No comments