SIMBA WASEMA WALIJUA KUWA KESSY ATAIDHINISHWA KUICHEZEA YANGA


Uongozi wa klabu ya Simba umesema kwamba wao walikua wanafahamu jambo hilo kua lazima TFF wamuidhinishe Kessy kucheza Yanga kwa sababu ndani ya shirikisho hilo asilimia kubwa ya viongozi ni mashabiki wa Yanga

Manara amesema kwamba anashangaa kuona TFF inalifanyia kazi jambo hilo kwa haraka zaidi ilihali kuna malalamiko yao ya muda mrefu yapo katika shirikisho hilo lkn hawayafanyii kazi.

Amesema kwamba mfano mzuri ni swala la Ramadhani Singano,Dornad Ngoma pamoja na Amisi Tambwe kesi za wachezaji hawa ni za muda mrefu lkn hakuna maamuzi yeyote ambayo yametolewa hadi ligi imemalizika na msimu mpya unataraji kuanza siku ya jumamosi

Hata hivyo amedai kua kama wao viongozi wa Simba watakaa na kulijadili swala hilo kama kutakua na namna basi watalitolea ufafanuzi katika maslahi ya klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa msimbazi K/koo jijini Dar es salaam.

No comments