MANJI ASEMA BASI INATOSHA KUIONGOZA YANGA AAMUA KUBWAGA MANYANGA


Mwenyekiti wa klabu ya Yanga,Yusuph Manji ameshindwa kusibitisha ukweli wa taarifa ambazo zimeenea kwenye mitandao ya kijamii  na taarifa kutoka kwa watu wake wa karibu juu  ya kujiuzuru kwake kuiongoza timu ya Yanga na kusitisha mpango wake wa kutaka kuikodisha timu hiyo kwa miaka 10.

Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa hii inasema kwamba Manji ameshindwa kuweka bayana juu ya jambo hilo isipokua alipoulizwa mpango wake wa kujiuzuru  aliishia kusema kwamba basi inatosha na hii ikionekana kama kauli ya kuachana na Yanga

Aidha kumekua na taarifa kwamba matajiri mbalimbali ambao ni wafanya biashara akiwemo Mengi wameanza kujitokeza kutaka kuisaidia timu hiyo endapo kama Manji ataamua kujiuzuru wadhifa huo


Hata hivyo taarifa zaidi zinasema kwamba Manji amemua kujiondoa Yanga baada ya kuzongwa na baadhi ya wanachama wa Yanga na viongozi wa serikali ambao wengi weo hawataki kuona mwenyekiti huyo anapata fursa ya kuikodisha timu hiyo kwa miaka 10.




No comments