NDANDA WATAMBA KUIFUNGA SIMBA SIKU YA JUMAMOSI



Uongozi wa timu ya soka ya Ndanda ya mkoani Mtwara umesema kwamba kikosi chao wakati wowote kinataraji kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya timu ya soka ya Simba,mchezo ambao unataraji kuchezwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa.

Msemaji wa timu hiyo,Idrisa Bandali amesema kwamba kwa sasa kikosi chao kinaendelea vyema na maandalizi ya mchezo huo wa ligi kuu ya Tanzania bara na wana matumaini makubwa ya kufanya vyema katika mechi yao dhidi ya Simba.

Amesema kwamba wanaamini mechi hiyo itakua na ushindani mkubwa na mara nyingi hua wanapokutana na Simba hua hawapati matokeo mazuri lkn kuelekea mchezo huo wamejipanga kikamilifu.

Hata hivyo Bandali amewataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuiunga mkono kwenye ushiriki wao wa ligi kuu ili timu hiyo ifanikiwe kufanya vizuri.

No comments