VIONGOZI WA MATAWAI WAMKATAA AKILIMALI WATAKA ASIMAMISHWE UWANACHAMA
Baadhi ya viongozi wa matawi wa klabu ya Yanga mkoa wa Dar es salaam pamoja na wanachama kwa pamoja wametoa lawama zao kwa katibu mkuu wa baraza
la wazee wa klabu hiyo,Ibrahim Akilimali kwa kusema kwamba katibu huyo ndiye
anayeleta mvuragano kwenye timu hiyo kufuatia kutoa kauli za uchochezi kwenye
vyombo vya habari hasa zikimlenga mwenyekiti wao Yusuph Manji
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari kaimu mwenyekiti
wa kanda zote za Dar es salaam Robert Ilyungukasere amesema kwamba kama wao
viongozi wa matawi wameamua kufanya hivyo baada ya kuwepo kwa taarifa za kutaka
kujiuzulu kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji na kusitisha mpango wake wa
kutaka kuikodisha timu kwa miaka 10
Amesema kwamba kwa sasa kwa pamoja wameutaka
uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa katibu mkuu wa klabu kumuondoa Akilimali
katika wadhifa wake wa kua katibu mkuu wa baraza la wazee kwa kua yeye ndio
kikwazo kikubwa kwa sasa kuhusiana na swala hili ambalo limemuhudhunisha Zaidi Manji
Nae mwenyekiti wa tawi la mwembe Yanga, Jamali
Tail ameutaka uongozi wa klabu hiyo kumfuta uwanachama wa klabu hiyo Ibrahim
Akilimali kwani amekua hana msada ndani ya klabu hiyo isipokua amekua akileta
mvurugano kwa vipindi tofauti
"Akilimali ashawai kutoa kauli yake ambayo ikapelekea tukafungwa goli tano na simba na leo hii ameendea kuleta mgogoro wakati kesho tuna mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Azam" alisema Jamal Tail.
Amesema kwamba Akilimali amekua akizungumza
kauli ambazo mara nyingi zimekua na athari kubwa kwa timu ikiwemo hivyo jambo
zuri la kufanya kwa sasa ni kutomtambua katibu huyo kama ni kiongozi wa Yanga
kupitia baraza la wazee
Aidha amemtaka mwenyekiti wa klabu Yusuphu
Manji kupuuzia jambo hili kwani mara nyingi hua mwadamu hakubaliki na watu wote
ingawa anafanya jambo jema.
Post a Comment