BAADA YA KUFUNGWA NA AZAM MASHABIKI YANGA WASEMA UCHOVU KWA WACHEZAJI WAO NDIO SABABU




Baada ya kufungwa na timu ya Azam FC katika mchezo wa ngao ya Hisani,baadhi ya mashabiki wa klabu ya Yanga wamesema kwamba licha ya kufungwa kwa jumla ya mikwaju ya penati 4-1 lkn kikosi chao kimecheza vizuri na hakipaswi kulaumiwa kwa kutoibuka na ushindi ingawa walianza kuongoza kwa 2-0 katika kipindi cha kwanza.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT mmoja wa mashabiki hao aliyejitambulisha kwa jina la Almas Said amesema kwamba kufungwa kwao katika pambano hilo ni kutokana na wachezaji kucheza mechi nyingi za kimashindano bila kupumzika hivyo kusabisha wachezaji kua na uchovu.

"Ujue sisi wachezaji wetu inawezekana wamechoka maana wamecheza mechi nyingi za kimashindano tofauti na wenzetu lkn wamecheza vizuri" 

Mchezaji Hassani Kessy pamoja na Haruna Niyonzima wamekosa kwa upande wa Yanga huku mlinda mlango Deogratius Munishi akifanikiwa kukwamisha wavuni penati ya kwanza akimfunga Aishi Manula.

No comments