YANGA KUWAFUATA TP MAZEMBE JUMAPILI KWA AJILI YA MECHI YA KUKAMILISHA RATIBA


Kikosi cha timu ya soka ya Yanga siku ya jumapili kinataraji kuelekea Lubumbashi Congo tayari kwa mchezo wao wa kukamilisha ratiba ya hatua ya makundi katika kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka idara ya habari ndani ya klabu ya Yanga zinasema kwamba mchezo huo unataraji kupigwa siku ya jumanne ya tarehe 23 mwezi huu sasa nane na nusu mchana kwa saa za Congo.

Baada ya kumaliza mechi ya jana ya ngao ya hisani kikosi cha Yanga kitaendelea na mazoezi kesho na keshokutwa kabla ya kuanza safari ya kuwafuata TP Mazembe waliyokata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika kwa nagazi ya vilabu.

Mwamuzi wa pambano hilo ni Helda Martins De Carvalho kutoka Angola akisaidiwa na Jean Claude Birumushashu kutoka Burundi,Arsenio Chadreque Marengula[Mozambique] Antonio Muachihussa Caxala [Angola] M.C Georges Rodolphe Bibi [Seylsius] R.A All Mohamed Ahmed [Somalia] GC Russell Paul kutoka Rep.of South Africa.

No comments