SIMBA WAJIANDAA KUPELEKA BARUA TFF KUFAHAMU TARATIBU ZILIZOTUMIKA HADI KESSY ANACHEZA YANGA


Uongozi wa timu ya soka ya Simba umesema kwamba upo katika mchakato wa kuliandikia barua shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF kuhusiana na shirikisho hilo kuiluhusu klabu ya Yanga kumtumia mchezaji Hassan Ramadhani Kesy katika pambano la jana la ngao ya Hisani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha taarifa hii kinasema kwamba uongozi wa Simba umeshangwazwa na hatua hiyo ya TFF kumuidhinisha Kessy aichezee Yanga kwa mechi ya jana ili hali mchezaji huyo amekiuka taratibu za mkataba baada ya kuanza kuitumikia Yanga wakati mkataba wake umekua haujaisha.

"Tunashangaa kuona TFF inafanya jambo kama hili la kumruhusu Kessy acheze Yanga wakati mchezaji na klabu husika zimekiuka taratibu za mkataba sijui haya maamuzi wameyatoa wapi"kilisema chanzo cha taarifa hii.

No comments