MGOSI ASEMA SIMBA ITAIFUNGA NDANDA JUMAMOSI TAIFA



Meneja wa timu ya Simba Musa Hassani Mgosi amesema kwamba wanaamini watafanya vizuri katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Ndanda mechi ambayo inataraji k kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya jumamosi

Mgosi ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba wachezaji wote wapo katika hali nzuri hivyo matumaini ya kuibuka na ushindi ni makubwa hasa baada ya kufanya maandalizi mazuri chini ya kocha Joseph Omog.

"Msimu huu tuko vizuri sana si unaona usajili ambao umefanywa na uongozi na maandali tuliyofanya kabla ya ligi kuaanza naamini Ndanda hatoki hiyo jumamosi"alisema Mgosi 
Amesema kwamba kikosi chao msimu huu kimekamilika kila idara tofauti na msimu uliopita kwani kila mchezaji ana molari ya hali ya juu sambamba na kuwa na viwango bora.

Hata hivyo Mgosi amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika pambano hilo ili kuwapa hamasa ya kutosha kwani timu ya Ndanda ni nzuri na hua wanaleta ushindani wa hali ya juu wanapokutana na Simba.

No comments