MANARA AKATAA SIMBA NA YANGA KUITWA MAHASIMU WA JADI
Na,Said Ally
Mkuu wa Idara ya Habari na mawasiliano ndani ya klabu ya Simba,Haji Manara amewataka watanzania kuacha dhana ya kuwaita Simba na Yanga kuwa ni mahasimu wa jadi.
Manara alisema kwamba Simba na Yanga sio mahasimu wa jadi kama inavyoelezwa na baadhi ya wadau wa soka,kwani ushabiki wa timu hizo haujafikia kuleta madhara makubwa kwa mashabiki wake.
Alisema kwamba wao ni watani wa jadi katika soka la Tanzania hasa kutokana na ukongwe wao na uwepo wa idadi kubwa ya mashabiki katika timu hizo.
Aidha katik hatua nyingine Manara alisema kwamba kikosi cha timu hiyo kimesharejea jijini Dar es salaam,kikitokea mkoani Morogoro kilipoweka kambi kwa ajili ya kujiwinda na mechi yao dhidi ya Yanga.
Kulekea kwenye mchezo huo utakaopigwa siku ya jumapili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,Manara alisema kwamba wachezaji wote wa Simba wako vizuri kwa ajili ya pambano hilo ambalo anaamini litakuwa na ushindani wa hali ya juu kutoka kwa pande zote mbili.

Post a Comment