MKWASA;MKONGOMANI ATAIPA MAFANIKIO YANGA

Kocha Zahera Mwinyi Mkongomani leo hii anatarajiwa kuwepo mkoani Morogoro kwa ajili ya kukutana na wachezaji pamoja na viongozi wengine wa benchi la ufundi,ili kuzungumza maahache kabla ya kurejea  jijini Dar kukamilisha taratibu za kuanza majukumu yake.

Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema kwamba alikutana na Kocha Mwinyi kwa ajili ya kutambuana na kufanya mazungumzo mafupi, na baadae kocha huyo  kuomba kukutana na wachezaji pamoja na viongozi wengine wa benchi la ufundi.

"Tumemruhusu kukutana na timu,apate baadhi ya kujua baadhi ya mambo kutoka kwa vijana na viongozi wengine wa benchi la ufundi,baada ya hapo atarejea  Dar kuja kukamilisha taratibu za kuanza majukumu ikiwa ni pamojana na mambao ya mikataba"alisema Mkwasa.

Mkwasa alisema kuwa mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga wanapaswa kufahamu kuwa kocha ni mzuri na amekuwa na mafanikio kwenye timu nyingi ambazo amezifundisha na pia amewai kufanya kazi na makocha wakubwa sehemu mbalimbali hivyo anaimani ataipa mafanikio klabu hiyo.

Ujio wa kocha huyo unafunga mjadala wa kocha George Lwandamina aliyeikacha timu hiyo ya Yanga na kutimkia katika klabu yake ya zamani ya Zesco United ya nchini Zambia.

No comments