KESI YA VIONGOZI WA SIMBA YAIVA,APRIL 30 KUSOMEWA MAELEZO YA AWALI
Na,Unique Maringo
Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili viongozi wakuu wa Simba,Rais Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange Kaburu imeahirishwa hadi april 30 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
Shauri hilo limeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mahakama ya Kisutu Mathar Mpanze, jijini Dar es Salaam,baada ya Mwendesha mashitaka wa serikali kutoka TAKUKURU Leonard Swai kudai shauri hilo limefika mbele yake kwa ajili ya kuahirishwa kutokana na Hakimu anaesikiliza shauri hilo kutokuwepo mahakamani.
Aidha hakimu Mpanze ameridhia na ukupanga shauri hilo kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali Aprili 30 2018
Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano ya uhujumu uchumi ikiwemo kughushi,kuwasilisha nyaraka ya uongo na utakatishaji fedha ambazo ni dola za Marekani (USD) 300,000.

Post a Comment