KAULI YA MWENYEKITI WA KAMATI YA WAAMUZI KUHUSIANA NA YANGA KUPEWA POINTI TATU

Na,Said Ally
Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi,Salum Umande Chama amesema kwamba matokeo ya mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara kati ya Yanga na Mbeya City yatabaki kama yalivyo licha ya kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa Yanga.

Chama ameiambia MWANDIKE BLOG,kwamba malamiko ya klabu ya Yanga kama yatakuwa na ukweli basi hatua za kisheria zitachukuliwa baada ya kupitia taarifa ya mwamuzi.

Alisema kwamba kama mchezji aliyeonyeshwa kadi nyekundu alirejea uwanjani kwa mara nyingine na kushangilia goli basi anastahili kupata adhabu, ambapo anaweza kufungiwa au kulipa faini ama akapewa adhabu zote kwa pamoja.

Aidha aliongeza kwa kusema kwamba,maamuzi ya mchezo huo yataamuliwa na kamati ya saa 72 baada ya kupata taarifa kutoka kwa mwaamuzi na msimamizi wa mchezo lakini hata hivyo maamuzi yake hayataweza kubadilisha matokeo ya mchezo hata kama itabainika Mbeya City walikuwa wengi uwanjani.

Kwa undani wa habari hii ungana nami katika kipindi cha Duru za michezo 98.1 Wapo Radio FM kuanzia mishale ya saa 12 na nusu jioni hadi saa moja kasoro dk 5 usiku.utasikia mengi kutoka kwa wachambuzi,viongozi na wadau wa soka juu ya swala hili.

No comments