YANGA WAKO TAYARI KUWAVAA MBEYA CITY

BAADA ya safari ya saa chache  kwa ndege wakitokea jijini Dar es Salaam, Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu
Tanzania bara, Yanga, leo wanashuka kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya wenyeji Mbeya City Fc.

Meneja Hafidh Saleh amesema kuwa nyota wote 20 waliosafiri tayari kwa mchezo wa leo wako na hali nzuri kiafya kinachosubiriwa ni heshima ya dakika 90 za uwanjani katika kutafuta pointi tatu muhimu. 

Hafidh alisema kuwa wachezaji Ibrahim Ajib na Andrew Vicent waliokuwa nje ya kikosi kupisha majeraha, tayari wamerejea kwenye hali nzuri kiafya hivyo kutumika linabaki kuwa suala la benchi la ufundi.

No comments