MTIBWA SUGAR WAFAFANUA USHIRIKI WA MICHUANO YA KIMATAIFA

Mtibwa Sugar Sports Club Ijumaa iliyopita ilifanikiwa kutinga fainali ya kombe la shirikisho  (Azam Sports Federation Cup) baada ya kuwaondosha Stand United kwa goli 2 kwa bila katika mchezo wa nusu fainali.
Mpinzani wa Mtibwa Sugar katika fainali hiyo tayari anajulikana ambaye ni Singida United ambaye  alimfunga JKT Tanzania kwa goli 2-1.
Mchezo huo wa fainali unatarajiwa kuchezwa katika jiji la Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid tarehe 2.06.2018, Mtibwa Sugar Sports Club wao wamesema wanajiandaa kutwaa ubingwa ili kuweza kupata nafasi ya kuwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa.
tunajiandaa kutoa support na kuwapa maandalizi bora wachezaji wetu kuelekea mchezo ujao wa fainali, tunataka kutwaa ubingwa wa kombe hilo ili kuweza kupata nafasi ya kuwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa” Swabur Abubakar
Pia katibu huyo msaidizi alizungumzia propaganda ambazo zilikuwa zinaenezwa kwamba Mtibwa Sugar imefungiwa katika michuano ya kimataifa
“ni kweli tuliwahi kufungiwa lakini adhabu ilisha malizika, tulifungiwa mwaka 2003 na adhabu hiyo ilikuwa inaisha mwaka 2007, wadau wakae wakijua tukifanikiwa kufuzu Insha Allah tutashiriki hatuna adhabu ya kutumikia kwakuwa tushamaliza kumekuwa na maneno kuwa ili utumikie adhabu hiyo lazima ufuzu ni uongo” Swaburi Abubakar
Mtibwa Sugar  Sports Club V Azam fc
Jumamosi hii ya tarehe 28, kikosi cha Mtibwa Sugar Sc   kinataraji kushuka uwanjani kukabiliana Azam fc katika mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League).
Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa nyumbani wa Mtibwa Sugar ambao ni Manungu Complex uliopo Turiani siku ya Jumamosi (28.04.2018).
Source;Mtandao wa Mtibwa Sugar.

No comments