MTIBWA SUGAR KUWAVAA AZAM FC

Wafalme wa soka kutoka mji kasoro bahari Mtibwa Sugar Sports Club Jumamosi ya tarehe 28.04.2018 hii wanataraji kuvaana na Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League).
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa nyumbani wa Mtibwa Sugar ambao ni Manungu, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 8:00 mchana.
Mtibwa Sugar Sports Club na Mtibwa Sugar wamekutana mara mbili msimu huu na wametoka sare michezo yote miwili iliyochezwa katilka uwanja wa Azam Complex, mchezo wa kwanza ulikuwa wa ligi kuu bara na uli isha kwa sare  ya 1-1 na mchezo wa pili ulikuwa wa kombe la shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na Mtibwa Sugar ili ibuka na ushindi wa penalti 8-9 baada ya dakika 90′ kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Mtibwa Sugar hadi sasa imefanikiwa kukiusanya pointi 33 baada ya kufanikiwa kucheza michezo 24 huku Azam Fc ikifanikiwa kukusanya pointi  46 baada ya kucheza michezo 25.

No comments