KAMATI YA UCHAGUZI TASMA YASIMAMISHA UCHAGUZI

Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Wataalamu wa Tiba ya Wanamichezo (TASMA),imehairisha uchaguzi wa Chama hicho uliokuwa ufanyike kesho Jumapili Aprili 29, 2018 mpaka hapo itakapotangazwa tena.
Kamati hiyo ya uchaguzi wa TASMA chini ya Mwenyekiti wake Leslie Liunda imesema sababu kubwa ya kuhairishwa kwa uchaguzi huo ni kamati ya utendaji kushindwa kutekeleza mahitaji ya msingi ya maandalizi ya uchaguzi husika.
Moja kati ya yale yaliyoshindwa kutekelezeka ni pamoja na kukosekana kwa fedha ya kuendeshea uchaguzi huo.
Kutokana na sababu hizo Kamati imehairisha uchaguzi mpaka pale Kamati ya Utendaji ya TASMA na kamati ya uchaguzi itakapo kaa tena kupanga tarehe mpya ya Uchaguzi


No comments