AMMY NINJE AWAPA MAPUMZIKO WACHEZAJI WAKE

Na Said Ally
Timu ya Taifa ya vijana Ngorongoro Heroes imerejea hapa nchini leo hii ikitokea nchini Dr Congo ilipokwenda kushiriki mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 20.

Afisa Habari wa TFF,Clford Mario Ndimbo alisema kwamba baada ya kurejea hapa nchini kocha wa timu hiyo Ammy Ninje aliwapa wachezaji mapumziko ya siku tatu kabla ya kurejea kambini kuendelea na maandalizi ya kujiwinda na mchezo wa raundi ya pili dhidi ya Mali.

Ndimbo alisema kwamba michezo yote ya raundi ya pili inatarajiwa kuchezwa mwezi mei huku kikosi cha timu hiyo ya vijana kitaanza kurusha karata yake nyumbani.

Katika hatua nyingine kikosi cha timu ya vijana ya Serengeti Boys hapo kesho kinataraji kushuka dimbani kumenyana na Kenya katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya CECAFA kwa vijana inayoendelea nchini Burundi.

Kwa mujibu wa Afsa Habari wa TFF,Clford Mario Ndimbo alisema kwamba shirikisho la soka hapa nchini linawaombea kila la kheri vijana hao ili wafanikiwe kufanya vizuri kwenye mchezo huo ili waweze kuingia fainali na hatmae kuwa mabingwa wa michuano hiyo ili kuleta heshima kwa Taifa.

No comments