WAZIRI WA KILIMO KUIONGOZA SIMBA IKIIVAA AL MASRY

Waziri wa kilimo wa Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Charles Tizeba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ambae ataongoza maelfu ya wanasimba na watanzania kuishangilia timu hiyo kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry ya Misri mchezo utakaoanza saa kumi na mbili jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa uongozi wa timu ya soka ya Simba umesema kwamba maandalizi kwa upande wao yanaenda vizuri na Makocha Hossam Hassan wa Timu ya Al-Masry na Pierre Lechantre wa Simba kesho saa tano asubuhi watazungumza na Wanahabari Kuelekea mchezo wao wa kombe la Shirikisho utakaopigwa siku ya Jumatano ya tarehe saba mwezi huu.



No comments