AJIBU AWAPA MOYO WANA YANGA

Na Said Ally
Kiungo mshambuliaji wa timu ya soka ya Yanga Ibrahim Ajibu amesema kwamba kikosi cha timu hiyo bado kina nafasi ya kushinda katika mchezo wao dhidi ya Township Rollers ya nchini Botswana na kufanikiwa kuingia katika hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Ajibu amesema kwamba licha ya kupoteza mechi yao ya nyumbani kwa kufungwa kwa jumla ya magoli 2-1 lakini anaamini nafasi bado wanayo ya kusonga mbele.

"Bado nafasi tunayo tunaweza na nina imani tutawapiga mbili hadi tatu kwao huko huko"alisema Ajibu.

Katika mchezo huo utakaopigwa nchini Botswana itawalazimu Yanga kupata ushindi wa mabao 2-0 au ushindi wowote utakaoanzia mabao 3 ndio ifanikiwe kufuzu katika hatua ya makundi kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

No comments